7Je, Mungu atanikataa milele? Je, hatanionesha tena huruma?
8Je, uaminifu wa agano lake ulikuwa umetoweka milele? Je, ahadi yake imeshindwa milele?
9Je, Mungu amesahau kuwa mwenye neema? Je, hasira yake imeifunga huruma yake? Selah
10Nilisema, “Hii ni huzuni yangu: mabadiliko ya mkono wa kuume wa Aliye Juu dhidi yetu.”
11Lakini nitayakumbuka matendo yako, Yahwe; nitafikiri kuhusu matendo yako makuu yaliyopita.
12Nitayatafakari matendo yako yote nami nitayaishi.
13Njia yako, Mungu, ni takatifu; ni mungu gani wa kulinganishwa na Mungu wetu aliye mkuu?