15Uliwapa watu wako ushindi kwa uweza wako mkuu - ukoo wa Yakobo na Yusufu. Selah
16Maji yalikuona wewe, Mungu; maji yalikuona wewe, nayo yakaogopa; vina vya maji vilitetemeka.
17Mawingu yalitiririsha maji chini; anga zito lilitoa sauti; mishale yako ilipita kati.
18Sauti yako kama ya radi ilisikika katika upepo; radi iliwasha dunia; nchi iliogopa na kutetemeka.
19Njia yako ilipita baharini na mapito yako katika maji mengi, lakini alama za miguu yako hazikuonekana.
20Uliwaongoza watu wako kama kundi kwa mkono wa Musa na Haruni.