16Mchana ni wako, na usiku ni wako pia; uliweka jua na mwezi mahari pake.
17Umeiweka mipaka ya nchi; umeumba majira ya joto na majira ya baridi.
18Kumbula vile adui alivyo vurumisha matusi kwako, Yahwe, na kwamba watu wapumbavu wamelitukana jina lako.
19Usimtoe njiwa afe kwa mnyama wa porini. Usiusahau milele uhai wa watu wako walio onewa.
20Kumbuka agano lako, maana majimbo ya giza ya nchi yamejaa maeneo ya vurugu.