Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 74

Zaburi 74:11-22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
11Kwa nini umerudisha nyuma mkono wako, mkono wako wa kuume? Utoe mkono wako kwenye mavazi yako na uwaangamize.
12Lakini Mungu amekuwa mfalme wangu tangu enzi, akileta wokovu tuniani.
13Wewe uliigawa bahari; ulishambulia vichwa vya majitu ya kutisha baharini majini.
14Wewe ulishambulia vichwa vya lewiathani; na kumfanya awe chakula cha viumbe hai jangwani.
15Ulizifungulia chemchem na vijito; uliikausha mito itiririkayo.
16Mchana ni wako, na usiku ni wako pia; uliweka jua na mwezi mahari pake.
17Umeiweka mipaka ya nchi; umeumba majira ya joto na majira ya baridi.
18Kumbula vile adui alivyo vurumisha matusi kwako, Yahwe, na kwamba watu wapumbavu wamelitukana jina lako.
19Usimtoe njiwa afe kwa mnyama wa porini. Usiusahau milele uhai wa watu wako walio onewa.
20Kumbuka agano lako, maana majimbo ya giza ya nchi yamejaa maeneo ya vurugu.
21Usiwaache walioonewa warudishwe kwa aibu; uwaache maskini na walioonewa walisifu jina lako.
22Inuka Mungu, itetee heshima yako; kumbuka wajinga wanavyokutukana machana kutwa.

Read Zaburi 74Zaburi 74
Compare Zaburi 74:11-22Zaburi 74:11-22