11Hakika wafalme wote wamwinamie yeye; mataifa yote yamtumikie yeye.
12Kwa kuwa yeye humsaidia mhitaji na maskini asiye na msaidizi.
13Yeye huwahurumia maskini na wahitaji, na huokoa maisha ya wahitaji.
14Huyaokoa maisha yao dhidi ya mateso na vurugu, na damu yao ni ya thamani machoni pake.
15Naye apate kuishi! Na dhahabu za Sheba apewe yeye. Watu wamuombee yeye siku zote; Mungu ambariki daima.
16Kuwepo na nafaka nyingi katika ardhi; juu ya milima kuwe na mawimbi ya mimea. Matunda yake yawe kama Lebanoni; watu wasitawi katika miji kama nyansi za kondeni.
17Jina lake lidumu milele; jina lake ilindelee kama vile jua ling'aavyo; watu wabarikiwe katika yeye; mataifa yote wamwite mbarikiwa.