5Maana wewe ni tumaini langu, Bwana Yahwe. Nimekuamini wewe siku zote tangu nilipokuwa mtoto.
6Nimekuwa nikisaidiwa na wewe tangu tumboni; wewe ndiye yule uliyenitoa tumboni mwa mama yangu; sifa zangu zitakuhusu wewe siku zote.
7Mimi ni mfano bora kwa watu wangu; wewe ni kimbilio langu lenye nguvu.
8Mama yangu atajawa na sifa zako, siku zote akikuheshimu.
9Usinitupe katika siku za miaka ya uzee wangu; usiniache wakati nguvu zangu zitakapoisha.