13Waaibishwe na kuharibiwa, wale walio adui wa uhai wangu; wavishwe laumu na kudharauliwa, wale watafutao kuniumiza.
14Lakini nitakutumainia wewe siku zote na nitakusifu wewe zaidi na zaidi.
15Kinywa changu kitaongea kuhusu haki yako na wokovu wako mchana kutwa, ingawa ziwezi kuzielewa maana ni nyingi mno.
16Nitakuja na matendo yenye nguvu ya Bwana Yahwe; nitataja haki yako, yako pekee.
17Mungu, tangu ujana wangu wewe umenifundisha; hata sasa ninatangaza matendo yako ya ajabu.
18Hakika, hata niwapo mzee na mvi kichwani, Mungu, usiniache mimi, kama ambavyo nimekuwa nikitanga nguvu yako kwa vizazi vijavyo, na uweza wako kwa yeyote ajaye.
19Pia haki yako, Mungu, iko juu sana; wewe ambaye umefanya mambo makuu, Mungu, ni nani aliye kama wewe?
20Wewe ambaye umetuonesha sisi mateso mengi utatuhuisha tena na utatupandisha tena juu kutoka kwenye kina cha nchi.
21Uiongeze heshima yangu; rudi tena na unifariji.
22Nami pia nitakushukuru kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako, Mungu wangu; kwako nitaimba sifa kwa kinubi, Mtakatifu wa Israel.