7Kwa ajili yako nimestahimili lawama; aibu imeufunika uso wangu.
8Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, nisiye fahamika wala kuaminika kwa watoto wa mama yangu.
9Kwa maana bidii ya nyumba yako imenila, na laumu zao wanao kulaumu wewe zimeniangukia mimi.
10Wakati nilipolia na kutokula chakula, walinitukana.
11Nilipoteneneza mavazi ya gunia, nikawa kituko kwao.
12Wale wakaao katika lango la mji huniseng'enya; mimi ni wimbo wa walevi.
13Lakini kwangu mimi, maombi yangu ni kwako, Yahwe, wakati ambao wewe utayapokea; unijibu katika uaminifu wa wokovu wako.
14Unitoe matopeni, na usiniache nizame; uniondoe mbali na wale wanaonichukia na uniokoe katika kina cha maji.
15Usiache mafuliko ya maji yanielemee, wala kina kisinimeze. Usiache mdomo wa shimo unimeze.
16Unijibu, Yahwe, maana uaminifu wa agano lako ni mwema; kwa maana rehema zako kwangu ni nyingi, unigeukie.
17Usiufiche uso wako mbali na mtumishi wako, maana niko katika dhiki; unijibu haraka.
18Uje kwangu na unikomboe. Kwa sababu ya adui zangu, uwe fidia yangu.
19Wewe wajua kulaumiwa kwangu, kuaibishwa kwangu, na kudharauliwa kwangu; wapinzani wangu wote wako mbele yako.
20Lawama imevunja moyo wangu; nimejawa na huzuni kubwa; nilitafuta mtu wa kunihurumia, lakini hakuwepo; nilitafuta wafariji, lakini sikupata.
21Walinipa sumu kwa ajili ya chakula changu; katika kiu yangu walinipa siki ninywe.
22Meza yao mbele yao na iwe mtego; wafikiripo wako kwenye usalama, iwe kitanzi.
23Macho yao na yatiwe giza ili kwamba wasiweze kuona; uvifanye viuno vyao kutetemeka daima.
24Wamwagie gadhabu yako, ukali wa hasira yako uwafikie wao.
25Sehemu yao na iwe ukiwa; mtu yeyote asiishi katika hema yao.
26Kwa kuwa walimtesa yule uliyempa adhabu. Mara kwa mara walihesabu maumivu ya wale walioumizwa.
27Wakiwashtaki kuwa wamefanya uovu juu ya uovu; usiwaache waje kwenye ushindi wa haki yako.
28Uwafute kwenye Kitabu cha Uzima na wasiandikwe pamoja na wenyehaki.
29Lakini mimi ni maskini na mwenye huzuni; uruhusu wokovu wako, Mungu, uniweke juu sana.
30Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo na nitamtukuza yeye kwa shukrani.
31Nitamsifu Yahwe zaidi kuliko ng'ombe au ndama aliye na mapembe na kwato.
32Wanyenyekevu wameona na kufurahi; ninyi mnao matafuta Mungu, mioyo yenu itiwe nguvu.