31Nitamsifu Yahwe zaidi kuliko ng'ombe au ndama aliye na mapembe na kwato.
32Wanyenyekevu wameona na kufurahi; ninyi mnao matafuta Mungu, mioyo yenu itiwe nguvu.
33Maana Yahwe husikia wenye uhitaji naye hawadharau wafungwa wake.
34Mbingu na nchi zimsifu yeye, bahari na vyote vitembeavyo majini.
35Kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na ataujenga tena mji wa Yuda; watu wataishi huko na kupata umiliki wao.