23Macho yao na yatiwe giza ili kwamba wasiweze kuona; uvifanye viuno vyao kutetemeka daima.
24Wamwagie gadhabu yako, ukali wa hasira yako uwafikie wao.
25Sehemu yao na iwe ukiwa; mtu yeyote asiishi katika hema yao.
26Kwa kuwa walimtesa yule uliyempa adhabu. Mara kwa mara walihesabu maumivu ya wale walioumizwa.
27Wakiwashtaki kuwa wamefanya uovu juu ya uovu; usiwaache waje kwenye ushindi wa haki yako.
28Uwafute kwenye Kitabu cha Uzima na wasiandikwe pamoja na wenyehaki.
29Lakini mimi ni maskini na mwenye huzuni; uruhusu wokovu wako, Mungu, uniweke juu sana.
30Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo na nitamtukuza yeye kwa shukrani.