2Imbeni utukufu wa jina lake; mzitukuze sifa zake.
3Mwambieni Mugu, “Matendo yako yanatisha kama nini! Kwa ukuu wa nguvu zako maadui zako watajisalimisha kwako.
4Nchi yote watakuabudu wewe na watakuimbia wewe; wataliimbia jina lako.” Selah
5Njoni na mtazame kazi za Mungu; yeye anatisha katika matendo yake awatendeayo wanadamu.
6Aligeuza bahari kuwa nchi kavu; wao walitembea kwa mguu juu ya mto; huko tulishangilia katika yeye.