1Kwako wewe, Mungu katika Sayuni, sifa zetu za kungoja; viapo vyetu vitaletwa kwako.
2Wewe usikiaye maombi yetu, miili yote itakuja kwako.
3Maovu yanatutawala sisi; kama yalivyo makosa yetu, wewe utayasamehe.
4Amebarikiwa mtu yule ambaye wewe huchagua kumsogeza karibu yako ili kwamba aishi hekaluni mwako. Tutatoshelezwa kwa uzuri wa nyumba yako, hekalu lako takatifu.
5Katika haki wewe utatujibu sisi kwa kufanya mambo ya ajabu, Mungu wa wokovu wetu; wewe ambaye ni ujasiri wa mwisho wote wa nchi na wa wale walio mbali toka pande za bahari.
6Kwa manaa ni wewe ndiye uliyeifanya milima imara, wewe ambaye umefungwa mkanda wa uweza.
7Ni wewe unyamazishaye ngurumo za baharini; ngurumo za mawimbi yake, na vurugu za watu.
8Wale wanaoishi sehemu za mwisho kabisa wa nchi wanaogopa ushahidi wa matendo yako; wewe hufanya mashariki na magharibi kushangilia.
9Wewe huja kuisaidia nchi; unainyeshea inchi; wewe unaiimarisha nchi vizuri; mto wa Mungu umejaa maji; wewe humpa mwanadamu nafaka unapokuwa umekwisha iandaa nchi.
10Wewe huyajaza matuta maji ya kutosha; wapasawazisha palipoinuka; wailainisha nchi kwa manyunyu ya mvua; waibariki mimea kati yao.
11Umeuvika mwaka taji ya wema wako; mvumo wa mapito yako hudondosha unono katika nchi.
12Majani ya nyikani hudondosha umande, na vilima vimevikwa furaha.
13Malisho yamevishwa mifugo; mabonde pia yamefunikwa na nafaka; yanapiga kelele za shangwe, nayo yanaimba.