2Hivyo nimekutafuta wewe katika watu watakatifu kuona nguvu zako na utukufu wako.
3Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakusifu wewe.
4Hivyo nitakutukuza wewe niwapo hai; kwa jina lako nitainua mikono yangu juu.
5Itakuwa kana kwamba nilikula mlo wa mafuta na wenye kunona, kwa midomo ya furaha kinywa changu kitakusifu wewe,
6nikufikiripo kitandani mwangu na kukutafakari wewe wakati wa saa za usiku.
7Kwa maana umekuwa msaada wangu, na katika uvuli wa mbawa zako ninafurahia.