3Waovu huenenda katika upotovu hata walipokuwa tumboni; wao wanaenenda katika upotovu tangu kuzaliwa, wakiongea uongo.
4Sumu yao ni kama sumu ya nyoka; wako kama fira kiziwi azibaye masikio yake,
5ambaye hasikilizi sauti ya waganga, haijalishi ustadi walio nao.
6Vunja meno yao midomoni mwao, Mungu; uyatoe meno ya mwana simba, Yahwe.
7Wayeyuke kama maporomoko ya maji; wafyatuapo mishale yao, iwe kama haina ncha.
8Wawe kama konokono ambaye huyeyuka na kutoweka, kama mtoto aliye zaliwa kabla ya wakati ambaye hakuona jua.