4Moyo wangu wasumbuka ndani yangu, na hofu ya kifo imeniangukia.
5Uwoga na kutetemeka kumenijia, nayo hofu imenielemea.
6Nikasema, “Oh, kama tu ningekuwa na mabawa kama njiwa! Ningelipaa mbali na kupata pumziko.
7Tazama, ningeenda mbali; ningekaa jangwani. Selah
8Ningefanya haraka kuja mafichoni mwako kuzikimbia dhoruba na tufani.”
9Uwaangamize, Bwana, vuruga lugha zao! Kwa maana nimeona vurugu na ugomvi katika mji.
10Mchana na usiku wao huenda kwenye kuta zake; uchafu na ufisadi uko katikati yake.