Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 55

Zaburi 55:2-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Unitazame kwa makini na unijibu; Sina pumziko katika shida zangu
3kwa sababu ya sauti ya adui zangu, kwa sababu ya ukandamizaji wa waovu; maana wananiletea matatizo na kunitesa wakiwa na hasira.
4Moyo wangu wasumbuka ndani yangu, na hofu ya kifo imeniangukia.
5Uwoga na kutetemeka kumenijia, nayo hofu imenielemea.
6Nikasema, “Oh, kama tu ningekuwa na mabawa kama njiwa! Ningelipaa mbali na kupata pumziko.
7Tazama, ningeenda mbali; ningekaa jangwani. Selah
8Ningefanya haraka kuja mafichoni mwako kuzikimbia dhoruba na tufani.”
9Uwaangamize, Bwana, vuruga lugha zao! Kwa maana nimeona vurugu na ugomvi katika mji.
10Mchana na usiku wao huenda kwenye kuta zake; uchafu na ufisadi uko katikati yake.

Read Zaburi 55Zaburi 55
Compare Zaburi 55:2-10Zaburi 55:2-10