Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 52

Zaburi 52:4-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Wewe hupenda maneno ambayo huwaumiza wengine, wewe ulimi mdanganyifu.
5Vivyo hivyo Mungu atakuadhibu wewe milele; yeye atakuchukua na kukuondoa katika hema yako na kukung'oa katika ardhi ya uhai. Selah
6Wenye haki pia wataona na kuogopa; watamcheka na kusema,
7“Tazama, huyu ni mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa kimbilio lake la usalama, bali aliamini katika wingi wa mali zake, naye alikuwa na nguvu alipowaharibu wengine.”
8Lakini kwangu mimi, niko kama mti bora wa mzeituni katika nyumba ya Mungu; Nami nitaamini uaminifu wa agano la Mungu milele na milele.
9Nitakushukuru wewe daima kwa uliyo tenda. Nitalisubiri jina lako, kwa sababu ni zuri, uweponi mwa wantu wako wa kimungu.

Read Zaburi 52Zaburi 52
Compare Zaburi 52:4-9Zaburi 52:4-9