13Je! sitakula nyama ya ngombe na kunywa damu ya mbuzi?
14Mtoleeni Mungu sadaka za shukurani, na mlipe viapo vyenu kwa Aliye Juu.
15Mniite katika siku ya shida; nami nitawaokoa
16Lakini kwa waovu Mungu anasema, “Inawahusu nini kuitangaza hali yangu, kwamba ninyi mmeliweka agano langu mdomoni mwenu,
17wakati ninyi mnayachukia maelekezo na mnayatupa maneno yangu?
18Mumuanapo mwizi, ninyi hukubaliana naye; ninyi na mnashirikiana na wale wafanyao uasherati.
19Mwautoa mdomo wenu kwa mabaya, huelezea udanganyifu.