5Kwa uweza wako tutawaangusha chini maadui zetu; kwa jina lako tutatembea juu yao, wale wanao inuka dhidi yetu.
6Kwa maana sitauamini upinde wangu, wala upanga wangu hautaniokoa.
7Bali wewe ndeye uliyetuokoa na adui zetu, na umewaaibisha wale watuchukiao.
8Katika Mungu tumefanywa kujivuna siku zote, nasi tutalishukuru jina lako milele. Selah
9Lakini sasa umetutupa na kutufedhehesha, na hauendi na majeshi yetu.