4Nami nilisema, “Yahwe unihurumie! Uniponye, kwa maana nimekutenda dhambi wewe.”
5Adui zangu huongea maovu dhidi yangu, wakisema, 'Atakufa lini na jina lake lipotee?'
6Adui yangu ajapo kuniona, huongea mambo yasiyo na maana; moyo wake hukusanya maafa yangu kwa ajili yake mwenyewe; na aondokapo kwangu, yeye huwaambia watu wengine kuhusu hayo.