17Kwa kuwa niko karibu mashakani, na niko katika maumivu ya mara kwa mara.
18Ninatubu makosa yangu; ninahuzunika kwa dhambi zangu.
19Lakini maadui zangu ni wengi; wale wanichukiao ni wengi.
20Wao wananilipa mabaya kwa mema; wanavurumiza shutuma kwangu ingawa nimefuata lililo jema.
21Usinitelekeze, Yahwe, Mungu wangu, usikae mbali nami.
22Njoo haraka unisaidie, Bwana, wokovu wangu.