Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 37

Zaburi 37:2-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Kwa kuwa muda mfupi watakauka kama nyasi na kukauka kama vile mimea ya kijani ikaukavyo wakati wa kiangazi.
3Uwamini Mungu na kufanya yaliyo mema; uishi katika nchi na uongezeke katika imani.
4Kisha ufurahi mwenyewe katika Yahwe, naye atakupa matamanio ya moyo wako.
5Umkabidhi njia zako Yahwe; uamini katika yeye, naye atatenda kwa niaba yako.
6Yeye ataidhihilisha haki yako kama mchana na usafi wako kama mwangaza wa mchana.
7Uwe kumya mbele za Yahwe na umsubiri yeye kwa uvumilivu. Usikasirike ikiwa kuna mtu anafanikiwa kwa kile afanyacho, au afanyapo njama za uovu.
8Usikasilile na kugadhabika. Usiogope. Hii huleta matatizo tu.
9Watendao maovu watafutiliwa mbali, bali wale wamngojao Yahwe watairithi nchi.

Read Zaburi 37Zaburi 37
Compare Zaburi 37:2-9Zaburi 37:2-9