19Hawata aibika siku mbaya zijapo. Wakati wa njaa ufikapo wao watakuwa na chakula cha kutosha.
20Bali waovu wataangamia. Maadui wa Yahwe watakuwa kama vile utukufu wa malisho; watamalizwa na kupotezwa katika moshi.
21Mtu mwovu hukopa lakini halipi, bali mtu mwenye haki ni mkarimu na hutoa.
22Wale walio barikiwa na Mungu watairithi nchi; wale aliowalaani watafutiliwa mbali.
23Hatua za mwanadamu zinaimarishwa na Yahwe, mtu ambaye njia zake zinakubalika machoni pa Mungu.