3Maneno yake ni yenye dhambi na udanganyifu; hataki kuwa mwenye hekima na kutenda mema.
4Alalapo kitandani, hupanga namna ya kutenda dhambi; yeye hukaa nje kwenye nja ya uovu; yeye hakatai uovu.
5Uaminifu wa agano lako, Yahwe, unafika mbinguni; uaminifu wako unafika mawinguni.
6Haki yako ni kama milima ya Mungu; hukumu yako ni kama kina kirefu. Yahwe, wewe huwahifadhi wote wanadamu na wanyama.
7Ni jinsi gani uaminifu wa aganao lako ni wa thamani, Mungu! Watu hukimbilia usalama chini ya uvuli wa mbawa zako.
8Nao watatoshelezwa tele na utajiri wa chakula nyumbani mwako; utawafanya wanywe kutoka katika mto wa baraka zako za thamani.