Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 35

Zaburi 35:8-22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Uharibifu na uwapate wao kwa kushitukiza. Mtego ambao wameutega na uwanase wao. Na wadumbukie humo, ili kwamba waangamizwe.
9Bali mimi nitakuwa nafuraha ndani ya Yahwe na ndani ya wokovu wake.
10Mifupa yangu yote itasema, “Yahwe, ni nani kama wewe, uokoaye walio onewa mkononi mwa walio na nguvu kuwazidi wao na masikini na wahitaji mkononi mwa wale wanaojaribu kuwaibia?”
11Mashahidi wa uongo wamesimama; wananishitakia uongo.
12Kwa ajili ya wema wananilipa mabaya. Nina huzuni nyingi.
13Lakini, walipokuwa akiugua, nilivaa magunia; nilifunga kwa ajili yao huku kichwa changu kikiinamia kifuani kwangu.
14Nilienenda katika huzuni kana kwamba walikuwa ni ndugu zangu; niliinama chini nikiomboleza kana kwamba ni kwa ajili ya mama yangu.
15Bali mimi nilipokuwa mashakani, walifurahi sana na kukutanika pamoja; walikutanika pamoja kinyume na mimi, nami nilishangazwa nao. Walinirarua bila kuacha.
16Kwa dharau kabisa walinidhihaki; walinisagia meno yao.
17Bwana, mpaka lini utaendelea kutazama? uiokoe roho yangu na mashambulizi yao ya maagamizi uyaokoe maisha yangu na simba.
18Nami nitakushukuru wewe katika kusanyiko kubwa; nitakusifu kati ya watu wengi.
19Usiwaache maadui zangu wadanganyifu kufurahi juu yangu; usiwaache waendelee na mipango yao ya uovu.
20Kwa maana hawaongei amani, bali wanabuni maneno ya uongo kwa wale wanaoishi kwa amani katika ardhi yetu.
21Midomo yao inapaza sauti ikinishtaki; wakisema, Aha, Aha, macho yetu yameona.”
22Yahwe wewe umeona, usikae kimya; Bwana, usiwe mbali nami.

Read Zaburi 35Zaburi 35
Compare Zaburi 35:8-22Zaburi 35:8-22