6Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote.
7Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa.
8Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.
9Muogopeni Yahwe, ninyi watu watakatifu wake. Hakuna kupungukikwa kwa wale wanao mhofu yeye.
10Simba wadogo wakati mwingine hukosa chakula na kuteseka kwa njaa, bali wale wamtafutao Yahwe hawatapungukiwa chochote kilicho kizuri.
11Njoni, wana, mnisikilize mimi. nitawafundisha ninyi hofu ya Yahwe.
12Mtu nani aliyepo ambaye anatamani maisha na anapenda kuwa na siku nyingi, ili kwamba aweze kuona vizuri?
13Hivyo uepushe ulimi wako na uovu na uilinde midomo yako kuongea uongo.
14Uache uovu na utende mema. Uitafute amani na kuiendea amani.
15Macho ya Yahwe yako kwenye haki na masikio yake huelekea kulia kwao.