18Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.
19Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote.
20Yeye huitunza mifupa yake yote, hakuna hata mmoja wao utavunjika.
21Uovu utawauwa waovu. Wale wachukiao haki watahukumiwa.