11Njoni, wana, mnisikilize mimi. nitawafundisha ninyi hofu ya Yahwe.
12Mtu nani aliyepo ambaye anatamani maisha na anapenda kuwa na siku nyingi, ili kwamba aweze kuona vizuri?
13Hivyo uepushe ulimi wako na uovu na uilinde midomo yako kuongea uongo.
14Uache uovu na utende mema. Uitafute amani na kuiendea amani.