1Furahini katika Yahwe, ninyi wenye haki; kusifu kwa wenye haki kwa faa sana.
2Mshukuruni Bwana kwa kinubi; mwimbieni sifa kwa kinubi chenye nyuzi kumi.
3Mwimbieni yeye wimbo mpaya; pigeni kwa ustadi na muimbe kwa furaha.
4Kwa kuwa maneno ya Mungu ni ya hakika, na kila afanyacho ni haki.
5Yeye hupenda haki na kutenda kwa haki. Dunia imejaa uaminifu wa agano la Yahwe.
6Kwa neno la Yahwe mbingu ziliumbwa, na nyota zote ziliumbwa kwa pumzi ya mdomo wake.
7Yeye huyakusanya maji ya baharini kama rundo; naye huiweka bahari katika ghala.
8Basi ulimwengu wote umwogope Yahwe; wenyeji wote wa ulimwengu wamuhofu yeye.