6Ninawachukia wale wanaotumikia miungu isiyo na maana, bali ninaamini katika Yahwe.
7Nitafurahi na kushangilia katika uaminifu wa agano lako, kwa kuwa uliyaona mateso yangu; wewe uliijua dhiki ya moyo wangu.
8Wewe haujaniweka kwenye mkono wa maadui zangu. Nawe umeiweka miguu yangu mahali pa wazi papana.
9Uniurumie, Yahwe, kwa maana niko katika dhiki; macho yangu yanafifia kwa huzuni pamoja na moyo wangu na mwili wangu.