13Kwa maana nimesikia minong'ono ya wengi, habari za kutisha kutoka pande zote kwa pamoja wamepanga njama kinyume na mimi. Wao wanapanga njama ya kuniua.
14Bali mimi ninakuamini wewe, Yahwe; Ninasema, “Wewe ni Mungu wangu.”
15Hatima yangu iko mikononi mwako. Uniokoe mikononi mwa maadui zangu na wale wanao nifukuzia.
16Nuru ya uso wako imuangazie mtumishi wako; uniokoe katika uaminifu wa agano lako.
17Usiniache niaibishwe, Yahwe; kwa maana ninakuita wewe! Waovu waaibishwe! Na wanyamaze kimya kuzimuni.
18Na inyamazishwe midomo midanganyifu ambayo husema maneno mabaya kuhusu watu wenye haki huku wakiwa na kiburi na dharau.
19Uzuri wako ni wa namna gani nao umeuhifadhii kwa ajili ya wale wanao kuheshimu sana, ambao wewe huufanya kwa ajili ya wale ambao hukimbilia kwako kwa ajili ya usalama mbele ya watoto wote wa wanadamu!
20Katika makao ya uwepo wako, wewe huwaficha mbali na njama za watu. Wewe huwaficha mahali salama na ndimi zenye vurugu.
21Atukuzwe Yahwe, kwa maana yeye alinionesha maajabu ya uaminifu wa agano lake mahali nilipoishi.
22Ingawa kwa haraka zangu nilisema, “Nimeondolewa machoni pako,” bali wewe ulisikia kusihi kwangu nilipokulilia wewe.