4Mwimbieni sifa Yahwe, ninyi waaminifu wake! Mshukuruni Bwana mkumbukapo utakatifu wake.
5Kwa kuwa hasira yake ni ya muda tu; bali neema yake yadumu milele. Kilio huja usiku, bali furaha huja asubuhi.
6Kwa ujasiri nilisema, “Sitatikiswa kamwe.”
7Yahwe, kwa neema yako uliniweka mimi kama mlima imara; lakini ulipouficha uso wako, nilisumbuka.
8Nilikulilia wewe, Yahwe, na kuomba msaada kwa Bwana wangu!
9Kuna faida gani katika kifo changu, kama nitaenda kaburini? Je, mavumbi yatakusifu wewe? Yatatangaza uaminifu wako?