6Abarikiwe Yahwe kwa sababu yeye amesikia sauti ya kusihi kwangu!
7Yahwe ni nguvu yangu na ngao yangu; moyo wangu wa humwamini yeye, na ninasaidiwa. Kwa hiyo moyo wangu hufurahia sana, nami nitamsifu yeye kwa kuimba.
8Yahwe ni nguvu ya watu wake, naye ni mkombozi salama wa wapakwa mafuta wake.