8Moyo wangu huongea kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Nami nautafuta uso wako, Yahwe!
9Usiufiche uso wako mbali na mimi; usinikasirikie mimi mtumishi wako! Wewe umekuwa msaada wangu; usiniache wala kunitelekeza, Mungu wa wokovu wangu!
10Hata kama baba yangu na mama yangu wakiniacha, Yahwe utanitunza kwako.
11Unifundishe njia yako, Yahwe! Kwa sababu ya adui zangu uniongoze katika njia salama.