3Asiaibishwe mtu yeyote anaye kutumaini bali waaibishwe wale watendao hila bila sababu!
4Unijulishe njia zako, Yahwe; unifundishe njia zako.
5Uniongoze kwenye kweli yako na unifundishe, kwa kuwa wewe ni Mungu wa wokovu wangu; ninakutumainia wewe siku zote za maisha yangu.
6Kumbuka, Yahwe, matendo yako ya huruma na uaminifu wa agano lako; kwa kuwa vimekuwapo siku zote.
7Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala uasi wangu; Uniweke akilini mwako pamoja na uaminifu wa agano kwa zababu ya uzuri wa wako, Yahwe!
8Yahwe ni mzuri na mwenye haki; kwa hiyo yeye huwafundisha njia mwenye dhambi.
9Yeye huwaelekeza wanyenyekevu kwa kile kilicho sahihi na yeye huwafundisha wao njia yake.