1Kwako, Yahwe, nayainua maisha yangu!
2Mungu wangu, ninaamini katika wewe. Usiniache niaibishwe; usiwaache maadui zangu wafurahie ushindi wao kwangu.
3Asiaibishwe mtu yeyote anaye kutumaini bali waaibishwe wale watendao hila bila sababu!
4Unijulishe njia zako, Yahwe; unifundishe njia zako.
5Uniongoze kwenye kweli yako na unifundishe, kwa kuwa wewe ni Mungu wa wokovu wangu; ninakutumainia wewe siku zote za maisha yangu.