Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 22

Zaburi 22:8-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Wao husema, “Yeye anamwamini Yahwe; mwache Yahwe amuokoe. Mwache amuokoe yeye, kwa kuwa yeye anampendeza sana Yeye.”
9Kwa kuwa wewe ulinileta kutoka tumboni; wewe ulinifanya nikuamini wewe wakati nikiwa nanyonya matiti ya mama yangu.
10Nimekwisha tupwa kwako wewe tokea tumboni; wewe ni Mungu wangu tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu!
11Usiwe mbali na mimi, kwa kuwa shida ikaribu; hayupo hata mmoja wa kusaidia.
12Maksai wengi wananizunguka mimi; maksai wenye nguvu ya Bashan wananizunguka mimi.
13Wao wanafungua midomo yao kwangu kama simba aungurumaye akirarua windo lake.
14Ninamwagwa nje kama maji, na mifupa yangu yote imeteguka. Moyo wangu ni kama nta; nao unayeyuka ndani ya sehemu zangu za ndani.

Read Zaburi 22Zaburi 22
Compare Zaburi 22:8-14Zaburi 22:8-14