14Ninamwagwa nje kama maji, na mifupa yangu yote imeteguka. Moyo wangu ni kama nta; nao unayeyuka ndani ya sehemu zangu za ndani.
15Nguvu zangu zimekaushwa kama kipande cha ufinyanzi; ulimi wangu unanata juu ya mdomo wangu. Wewe umenilaza mimi katika vumbi la mauti.
16Kwa maana mbwa wamenizunguka; kundi la watu waovu limenizunguka; wamenitoboa mikono yangu na miguu yangu.
17Nami ninaweza kuihesabu mifupa yangu. Wao wananitazama na kunishangaa.
18Wao wanagawa mavazi yangu kati yao wenyewe, wanapiga kura kwa ajili ya mavazi yangu.
19Usiwe mbali, Yahwe; tafadhali harakisha kunisaidia mimi, nguvu yangu!