Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 17

Zaburi 17:1-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Maombi ya Daudi. Sikia ombi langu kwa ajili ya haki, Yawhe; uusikilize mwito wangu wa msaada. Uyasikilize maombi yangu yatokayo katika midomo isiyo na udanganyifu.
2Uthibitisho wangu na uje kutoka uweponi mwako; macho yako na yaone kile kilicho sahihi!
3Kama utaujaribu moyo wangu, kama utakuja kwangu wakati wa usiku, wewe utanitakasa na hautapata mipango yeyote ya uovu; mdomo wangu hautavunja sheria.
4Kama kwa matendo ya binadamu, ni katika neno la midomo yako ya kuwa nimejiepusha na njia za wahalifu.
5Mwenendo wangu umeshikila kwa umakini mwenendo wako; miguu yangu haija teleza.
6Nakuita wewe, kwa kuwa unanijibu, Mungu; geizia sikio lako kwangu na usikilize ninapo ongea.
7Onyesha uaminifu wa agano lako katika namna ya ajabu, wewe uokoaye kwa mkono wa haki yako wale wanao kukimbilia wewe kutoka kwa adui zao.
8Unilinde kama mboni ya jicho lako; unifiche katika kivuli cha mbawa zako
9kutoka katika uwepo wa waovu ambao wananitusi, adui zangu wanizungukao.
10Wao hawana huruma kwa yeyote; midomo yao huongea kwa majivuno.

Read Zaburi 17Zaburi 17
Compare Zaburi 17:1-10Zaburi 17:1-10