1Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu za ukuu wake.
2Msifuni yeye kwa matendo yake makuu; msifuni yeye kwa kadri ya wingi wa ukuu wake.
3Msifuni kwa mlipuko wa pembe; msifuni kwa kinanda na kinubi.
4Msifuni kwa ngoma na kucheza; msifuni kwa vyombo vya nyuzi na filimbi.
5Msifuni kwa matoazi yavumayo; msifuni kwa matoazi avumayo sana.