1Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe, ninyi mlio katika mbingu; msifuni yeye, ninyi mlio juu.
2Msifuni yeye, enyi malaika wake wote; msifuni yeye, majeshi ya malaika wake wote.
3Msifuni yeye, enyi jua na mwezi; msifuni yeye, nyota zote zing'aazo.
4Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu zaidi na maji yaliyo juu ya anga.
5Na vilisifu jina la Yahwe, maana aliamuru, navyo vikaumbwa.