13Maana yeye huyakaza mapingo ya malango yako, huwabariki watoto wako kati yako.
14Huletamafanikio ndani ya mipaka yako, hukutosheleza kwa ngano bora.
15Huipeleka amri yake juu ya nchi, amri zake hupiga mbio sana.
16Huifanya theluji kama sufu, huitawanya barafu kama majivu.
17Hutupa mvua ya mawe kama makombo, ni nani awezaye kuhimili baridi aitumayo?