15Macho ya wote yanakungoja wewe; nawe huwapa chakula chao kwa wakati sahihi.
16Huufungua mkono wako na hukidhi haja ya kila kiumbe hai.
17Yahwe ni mwenye haki katika njia zake zote na neema katika yote afanyayo.
18Yahwe yu karibu na wote wamwitao, wale wamwitao yeye katika uaminifu.