10Vyote ulivyo viumba vitakushukuru wewe, Yahwe; waaminifu wako watakutukuza wewe.
11Waaminifu wako watanena juu ya utukufu wa ufalme wako, na watahubiri juu ya nguvu zako.
12Watayafanya matendo makuu ya Mungu ya julikane na wanadamu na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13Ufalme wako ni wa milele, na mamlaka yako ya dumu kizazi hata kizazi.
14Yahwe huwategemeza wote waangukao na huwainua wote walioinama chini.