8Ee Yahwe, usiyatimize matakwa ya waovu; usiruhusu njama zao kufanikiwa. Selah
9Wale wanao nizunguka huinua vichwa vyao; madhara ya midomo yao wenyewe na yawafunike.
10Makaa ya moto na yawaangukie; uwatupe motoni, kwenye shimo refu, wasiweze kuinuka tena.
11Watu wenye ndimi na wasifanywe salama juu ya nchi; na uovu umuwinde kumpiga mtu mwenye vurugu mpaka afe.