2Oh, Mshukuruni Mungu wa miungu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
3Oh, mshukuruni Bwana wa mabwana, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
4Mshukuruni yeye ambaye peke yake hufanya maajabu makuu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
5Yeye aliyezifanya mbingu kwa hekima zake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.