10Mshukuruni yeye aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa Misri, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
11Akawatoa Waisraeli kati yao, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
12Kwa mkono hodari na mkono ulio nyooshwa, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
13Mshukuruni yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
14Na kuwapitisha Waisraeli katikati yake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
15Lakini akamtupa Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
16Mshukuruni yeye aliye waongoza watu wake jangwani, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wa milele.
17Yeye aliyewaua wafalme wakuu, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wadumu milele.
18Mshukuruni yeye aliyewaua wafalme maarufu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
19Sihoni mfalme wa Waamori, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.