7Tutaingia katika maskani ya Mungu; tutasujudu miguuni pake.
8Inuka, Ee Yahwe, uje mahali pako pa kupumzika, wewe na sanduku la nguvu zako!
9Makuhani wako na wavikwe uadilifu; waaminifu wako washangilie.
10Kwa ajili ya mtumishi wako Daudi, usimuache mfalme wako uliye mpaka mafuta.
11Yahwe alimwapia Daudi kiapo cha uhakika, kiapo cha uhakika ambacho hatakivunja: “Nitamuweka mmoja wa wazawa wako kwenye kiti chako cha enzi.
12Kama wana wako watalishika agano langu na sheria ambazo nitawafundisha, watoto wao pia watakaa kwenye kiti chako cha enzi milele.”
13Hakika Yahwe ameichagua Sayuni, ameitamani kwa ajili ya makao yake.
14“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele. Nitaishi hapa, kwa kuwa ninapatamani.
15Nitapabariki sana kwa mahitaji. Nitawatosheleza maskini wake kwa mkate.
16Nitawavisha makuhani wake kwa wokovu, waaminifu wake watashangilia kwa furaha.
17Hapo nitachipusha pembe kwa ajili ya Daudi na kuweka taa juu kwa ajili ya mpakwa mafuta wangu.
18Nitawavisha adui kwa aibu, bali juu yake taji yake itang'aa.”