6Tazama tulisikia kuhusu hilo katika Efrata; tuliipata katika konde la Yearimu.
7Tutaingia katika maskani ya Mungu; tutasujudu miguuni pake.
8Inuka, Ee Yahwe, uje mahali pako pa kupumzika, wewe na sanduku la nguvu zako!
9Makuhani wako na wavikwe uadilifu; waaminifu wako washangilie.
10Kwa ajili ya mtumishi wako Daudi, usimuache mfalme wako uliye mpaka mafuta.