97Oh ni jinsi gani naipenda sheria yako! Ni tafakari yangu mchana kutwa.
98Amri zako hunifanya mwenye hekima kuliko adui zangu, maana amri zako siku zote ziko pamoja nami.
99Ninauelewa zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa maana ninazitafakari amri za agano lako.
100Ninaelewa kuliko wale wanaonizidi umri; hii ni kwa sababu nimeyashika maagizo yako.
101Nimeiepusha miguu yangu na kila njia ya uovu ili niweze kulitii neno lako.
102Sijaenda kinyume na amri zako za haki, kwa maana wewe umenifundisha.
103Ni jinsi gani maneno yako ni matamu kwenye majaribu yangu, naam, matamu kuliko asali kinywani mwangu!